Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini anayetetea kiti chake, Mchungaji Peter Msigwa ametoa sababu za kumuunga mkono mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa licha ya kuwa aliwahi kusema wanaofanya hivyo wanapaswa kupimwa akili.

Akijibu swali la mmoja kati ya wahudhuriaji katika mdahalo wa ‘Panga Pangua’ uliorushwa na Azam TV ukiwahusisha wagombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa alikiri kutoa kauli hiyo na kueleza kuwa alijipima na kuchekecha akagundua alikosea kufanya uamuzi huo wakati ule, na sasa amebaini ukweli na kuamua tofauti.

“Ni kweli mimi ni mchungaji na sio wa kubabaisha. Ni kweli nilisimama kwenye mkutano wa Mwembetogwa wakati huo nilikuwa nakaribishwa kutoka Bungeni nilisema uliyosema. Sasa swali lako unasema ‘je, wewe (Msingwa) umepimwa?’ “Nimepima, nimepimwa, nimechekecha nimeona Edward Ngoyai Lowassa ndiye anayefaa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mchungaji Msigwa.

“Kwahiyo nakushauri na wewe ukafikiri vizuri, na muungwana huwa anasema kuna wakati nilikosea kutoa maamuzi sasa nimerudisha. Sasa nasema kuwa nimepima na nimeona anafaa. Kwahiyo nikushawishi na wewe, rais bora baada ya rais kuondoka, katika wagombea wote ni Edward Lowassa,” aliongeza.

Ashley Young Aachwa Old Trafford
Jackson Mayanja Atimuliwa Barabara Ya 11