Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa amesema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi hana mamlaka ya kumuagiza chochote kwani yeye anapokea maagizo kutoka kwa wananchi.

Ameyasema hayo hii leo Agosti 22 wakati akizungumza na EATV&EARadio ikiwa ni baada ya RC Hapi kumtaka aitishe mkutano jimboni kwake ili awape wananchi taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

”Hapi anawezaje kuniagiza mimi, yeye kama nani, mimi naagizwa na wananchi, yeye hana mamlaka ya kuniagiza chochote labda mngemuuliza yeye ananiagiza kwa mamlaka ipi, hicho ni kitu hewa yeye si bosi wangu na wala hana hayo mamlaka kisheria, alikuwa anafurahisha genge tu,” amesema Msigwa

Kwa mujibu wa RC Hapi amedai kuwa CCM imefanya mambo makubwa Mkoani humo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi, lakini wananchi wamekuwa hawapewi taarifa hizo.

Kenya kuiwakilisha Afrika 'UN'
Ripoti ya CAG yaibua madudu TPB