Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa kwa tiketi ya Chadema amelaumiwa vikali na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani mara baada ya kutoa hutoba yake akimsifia Rais Magufuli katika utendaji wake, kufuatia lawama hizo Msigwa ameomba radhi kufuatia hotuba hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitwer Msigwa ameandika hivi.

”Ufafanuzi wangu bado haueleweki na heshima kuzingatia maumivu yenu. Kwa mkanganyiko huu. Nagundua rafiki zangu na wanachama wetu wanaugua. Basi niseme nini?  Naomba nisameheni sana. The couse we are fighting for is more important than my personality. I take responsibility”.

Aidha katibu wa Chadema Dar es salaam kuu na Mjumbe Baraza kuu na Mkutano Mkuu Taifa Chadema, Kileo Mwanga ameandika kwenye kurasa yake ya Twitter kuukubali msamaha wa Mhe. Msigwa.

Jana kupitia mitandao mbalimbai ya kijamii ilisambaa video ikimuonesha Mhe. Msigwa akihutubia na kumsifia Rais Magufuli juu ya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ambayo ameyawezesha hata katika mikoa ambayo wabunge wake ni kutoka vyama vya upinzani, Msigwa alisikika akisema Rais hapendelei ni wa watu vyote hata wa vyama vya pinzani.

”Umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali vyama, na hili limedhihirika kuwa hujali vyama, hela za kutoka kwako zimekuwa nyingi tuna barabara ya lami mradi wa World Bank kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu bilioni 3.5, tuna stendi nzuri, tuna maji, kwakweli  mheshimiwa Rais hupendelei hela zinakuja hata sisi ambao ni wa chadema unaleta hela, kwa hiyo wewe huwa hujali vyama”.

Hayo alizungumza Mbunge Peter Msigwa pindi Rais alipotembelea jimbo lake.

 

Ndalichako awaonya baadhi ya watumishi
Waandaaji tuzo za Oscar wawatumbua vigogo kwa ubakaji