Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limekataa ombi la kufanya mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji, Peter Msigwa kwa kile ilichokieleza kutokuwa na ulinzi wa kutosha.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Jeshi hilo kwenda kwa Mbunge Msigwa, imeeleza kuwa polisi wamepokea taarifa za Kiintelijensia ikieleza kuwa wamegundua uwepo wa vikundi vya watu ambao wamepanga kufanya vurugu kwenye mkutano huo.

Aidha sababu nyingine iliyoelezwa na Jeshi la Polisi, imedai kuwa imezuia mkutano huo kwa kutokuwa na askari wa kutosha ambao wengi wameelekezwa kwenda kusimamia, mitihani ya kidato cha nne na kidato cha pili.

Kwa mujibu wa barua ambayo aliandika Mchungaji Msigwa Novemba 19, Mbunge huyo alihitaji kufanya mkutano huo katika uwanja wa Mwembetogwa ambapo alihitaji uanze saa 8 mchana hadi saa 12 jioni.

Hata hivyo, Oktoba 9 mwaka huu Msigwa alisema kuwa alishikiliwa na Polisi kwa muda akitakiwa kutoa maelezo kwa kile walichodai kuwa ametoa lugha ya uchochezi kwenye mkutano wa hadhara.

 

Video: Diwani Urio aahidi neema kwa wahitimu wa ufundi Cherehani, Kunduchi Jijini Dar
20 mbaroni kwa kumteka mwanamke Muitaliano