Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mhe Peter Msigwa amewekwa ndani kwa saa chache na kupigwa marufuku na jeshi la polisi wilayani Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kuzungumza na wananchi wa jimbo la Iringa iliyoanza jana.

Katazo hilo ni kufuatia kile kilichodaiwa kuwa mkutano wake alioufanya jana eneo la Kihesa uliambatana na lugha za matusi na uchochezi kinyume na lengo ambalo alilitaarifu jeshi la polisi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Msigwa alipata kibali cha kufanya mikutano ya kuhamasisha maendeleo, kusikiliza kero za wananchi wa Iringa na kuzitafutia ufumbuzi.

”Polisi wameaniambia nitoe maelezo nimekataa , RCO akaniamrisha niwekwe ndani ndani nikamwambia Sawa! baadaye  wakaniambia tafuta mtu akudhamini nikawaambia sina mdhamini, wakaniambia nijidhamini nikakataa, baadaye wakasema Basi ondoka hapa hatukuhitaji tukitaka tutakuita, Ila nisiendele na mikutano!”amesema Msigwa.

e82d9883-271b-4450-8eac-41ef10307168-jpeg.891490

Inashangaza, binti ajioa mwenyewe aalika wazazi wake kushuhudia
Jeshi la Polisi Sudan Kusini labadilishwa jina