Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema msimamo wa Tanzania ni uleule wa kutoegemea upande wowote katika mzozo wa Urusi na Ukraine kama ilivyo kwa mataifa mengi barani Afrika ili kutoa nafasi ya diplomasia na kuzingatia mustakabali wa kiuchumi na kisiasa katika ulimwengu unaopitia mabadiliko makubwa.
Dk. Mpango amesema hayo wakati wa mkutano unaendelea katika Umoja wa nchi za Kiarabu Emirates kuwa “Tulijizuia kwa sababu tunataka ulimwengu kutoa nafasi ya diplomasia.”
Dk. Mpango amesema katika Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Dunia huko Dubai, akihusisha kura ya Machi 2 ya Tanzania kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya Azimio la kutaka Urusi ijitoe Ukraine.
Itakumbukwa kuwa Wanachama 141 wa Umoja wa Mataifa waliidhinisha azimio hilo, huku watano wakipinga na 35 hawakupiga kura zikiwemo nchi 17 za Afrika.
Marekani na washirika wake wamekuwa wakishinikiza mataifa mengine kujiunga na kampeni ya kuweiwekea Urusi vikwazo baada ya kusema hapo awali – kuhusu Ukraine – kwamba mataifa huru yana haki ya kuchagua kwa uhuru bila “kuonewa” na mataifa mengine.