Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya  Chadema, Mchungaji Peter Msigwa amekamatwa na jeshi la polisi mjini humo pamoja na watu 67 wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama hicho.

Duru kutoka mjini Iringa zinaeleza kuwa watu hao walikutwa katika moja kati ya hotel mjini humo ambapo inadaiwa kuwa walikuwa wakifanya kikao cha siri kilichokuwa kikiongozwa na Msingwa ambaye anagombea tena nafasi ya ubunge wa jimbo la Iringa Mjini.

Msigwaa

Aidha, inadaiwa kuwa Msigwa hakuwa katika eneo la hotel hiyo wakati polisi walipovamia na kuwakatama watu hao kwa kuwa alikuwa ametoka muda mfupi kabla ya tukio hilo. Hata hivyo, polisi walimkamata na kumuunganisha na watu wale 67.

Bado haijafahamika sababu hasa iliyopelekea kukamatwa kwa Msigwa na wafuasi wake.

Arsenal Kujaribu Bahati Ya Pili Ulaya
Picha: Muheza, Korongwe Wambeba Lowassa