Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ameeleza kuandika barua kwa uongozi wa Bunge, akishinikiza kulipwa mshahara na stahiki zake za Januari, lasivyo ataushtaki mahakamani uongozi wa Bunge baada ya ndani ya siku 14.

Akizungumzia barua yake kwa uongozi wa Bunge, amesema aliwaagiza mawakili wake kuwasiliana na uongozi wa Bunge ili kufahamu ni lini wataanza kumpatia tena mshahara wake na stahiki za kibunge.

“Mawakili wangu wamemwandikia barua Katibu wa Bunge, Kagaigai ya kumtaka kulipa mshahara na posho zangu za kibunge za tangu Januari mwaka huu. pia walimpa siku 14 kutekeleza madai, vinginevyo tutafungua madai Mahakama Kuu,”amesema Lissu.

Aidha, machi 14, 2019 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliibua madai ya kutoingizwa na mshahara wake na Mhimili wa Bunge madai ambayo Spika wa Bunge, Job Ndugai alijibu kuwa alipaswa kuuliza uongozi wa Bunge juu ya mshahara wake.

Akizungumza kuhusu mshahara wa Lissu, Ndugai alisema kuwa hajasikia lolote kuhusu madai ya mshahara na kwamba kama hajapata mshahara alitakiwa kufuata taratibu za ofisi ya bunge ili kujua tatizo.

Ofisi ya makamu wa Rais yapongezwa kwa jitihada za kutunza mazingira
Wafungwa Kenya wataka kuongezwa mshahara