Watumishi wa serikali na Wananchi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa kutofumbia macho suala la usalama kwa kutoruhusu wahamiaji haramu kuingia kiholela, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhatarisha amani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, amabpo amesema kuwa kuruhusu Wananchi kutoka Nchi jirani kuingia mkoani humo bila kufuata utaratibu uliowekwa kishera haikubaliki na hataruhusu hilo kutokea.

Bodi ya mikopo kufuta tozo kwa wanufaika

“Wananchi wote katika mkoa wanapaswa kushiriki kudumisha amani kwa kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika juu ya watu wanaoingia kinyemela ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi yao, wasikae na kuliacha suala hili kwa viongozi tu watambue nao linawahusu” amesema Jenerali Mbuge.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa mpya, ili kuhakikisha Mkoa huo unaendelea kuwa salama.

Mutafungwa awavalia njuga madereva wa malori
TFF yathibitisha timu nne kimataifa