Wakala wa Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp, Marc Kosicke amesisitiza kuwa kuwa mteja wake hataweza kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani licha ya jina lake kuwa miongoni mwa wanaotajwa kupewa mikoba ya timu hiyo.

Kosicke amesema kuwa dili hilo halitawezekana kwa kuwa Klopp ana mkataba wa muda mrefu na Liverpool na kwa sasa amejipanga kwa ajili ya timu hiyo pekee.

Klopp anatajwa kuwemo kwenye orodha ya majina ya makocha ambao wanahitajika kwa ajili ya kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani ambayo haina kocha kwa sasa baada kocha wake, Hansi Flick kufukuzwa.

Akizungumzia kuhusiana na suala hilo, Kosicke alisema: “Klopp hawezi kujiunga na Ujerumani kama kocha kwa sasa, anaendelea kujipanga na Liverpool pekee.

“Jurgen ana mkataba wa muda mrefu na Liverpool na hawezi kuusutusha ili akafanye kazi na Chama cha soka Ujerumani.,” alisema Kosicke.

Aubun Kramo akomalia kurudi kwao
Karia: Taifa Stars itavuka makundi AFCON 2023