Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela amesema Serikali inatakiwa kutambua dhana kuu ya Uongozi kwa kuhakikisha inatatua matatizo ya Wananchi na si kuzalisha Migogoro.

Kunchela ameyasema hayo Mkoani Katavi hivi karibuni nakuongeza kuwa endapo kiongozi atashindwa kufanya ivo ni wazi kuwa uwezo wake wa kuongoza ni mdogo, huku akiwataka Wananchi na Viongozi wa Serikali kutambua kuwa Mkoa huo si kitovu cha uhalifu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela.

Aidha, ameitaka Serikali kushirikiana na Wananchi katika kufanya maamuzi kwani sheria inawataka kufanya ivo na wasipo washirikisha wanaweza wasifikie malengo.

Hata hivyo Kunchela ameongeza kuwa Chadema ndio chama peke Tanzania kinachoaminiwa na kinachoweza kuwasemea Wananchi na Serikali ikasikia.

Giorgio Chiellini: Inatosha, ninajiweka pembeni
Sanga ataka ubunifu hamasa ya maendeleo Ardhi