Kikosi bora cha wachezaji kumi na mmoja kilichocheza hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kimetangazwa na Uefa jambo la kushangaza likiwa kuachwa nje kwa nyota wa Barcelona Lionnel Messi, Neymar na Luis Suarez.

Washambuliaji Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Hulk (Zenit St Petersburg) pamoja na Thomas Muller (Bayern Munich) ndio wanaoongoza safu ya ushambuliaji, kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.

Ligi Kuu ya Uingereza imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona, hawajatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji.

Kikosi kamili ni:

Kipa: Kevin Trapp (Paris Saint-Germain)

Mabeki: Andrea Barzagli (Juventus),Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Diego Godin (Atletico Madrid), David Alaba (Bayern Munich)

Viungo wa Kati: Sven Kums (Gent), Willian (Chelsea), Raheem Sterling (Manchester City)

Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Munich), Hulk (Zenit St Petersburg), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).

Waamuzi 18 Watajwa Kwa Ajili Ya EURO 2016
Dar es salaam Young Afrcans Wamalizana Na Paul Nonga