Uongozi wa Young Africans umesema mchakato mzima wa kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko wa klabu hiyo unasimamiwa na Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo kwa asilimia mia moja.

Mwenyekiti wa Young Africans Mshindo Mbette Msola amelianika suala hilo hadharani, alipozungumza na waandishi wa habari, Hotel ya Serena, jijini Dar es salaam mapema hii leo (Desemba 02).

Msolla ambaye aliongozana na viongozi wengine wa Young African kwenye mkutano huo amesema mchakato huo unaendelea vyema na mpaka sasa umepiga hatua kubwa.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka kampuni ya GSM Hersi Said na Alvaro Paya mwakilishi wa La Liga walikuwa nchini Hispania kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi rasimu ya awali ya uendeshwaji wa klabu.

Msola amesema kuwa kuna karatasi 400 ambazo zimezungumza kuhusu mchakato huo ambao utaleta mabadiliko ndani ya Yanga kwa kufuata sheria za Serikali.

Msola ameongeza kuwa walipaswa kufanya mkutano hivi karibuni ila walighairii kwa ajili ya mchakato huo ambapo leo makabidhiano ya rasmu hiyo imefanyika huku uongozi ukiwa umeanza kuandaa mpango kazi kwa ajili ya mkutano mkuu utakaoitishwa  hivi karibuni

Mshauri kwenye masuala ya mabadiliko, Senzo Mbatha amesema kuwa anaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa na watafikia malengo ambayo wanayahitaji.

Lwanga mali halali Simba SC
Uingereza kuanza kutoa chanjo ya Covid-19 wiki ijayo