Eminem amewekwa kitimoto kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kombora la mstari wa wimbo wake ‘Killshot’ kumtaja Diddy akimhusisha na sababu za kifo cha Tupac.
Katika wimbo huo ambao ameutoa kama majibu ya mashambulizi (diss track) kwa rapa Machine Gun Kelly, Eminem alitumia mfano wa tukio hilo akidai kuwa siku ambayo rapa huyo atatoa wimbo mkali (hit) ndipo siku ambayo Diddy atakiri kuwa alisababisha kifo cha rapa Tupac Shakur.
Akiwa na maana kuwa haitaweza kutokea Kelly kutoa wimbo mkali.
“Kellz, the day you put out a hit is the day Diddy admits that he put the hit out that got Pac killed,” anarap Eminem.
Hata hivyo, mwishoni mwa ngma hiyo anasikika akijaribu kuweka mambo sawa na Diddy akimueleza kuwa anaamini Diddy anajua anafanya utani lakini anampenda.
“You know I’m just playing Diddy, you know I love you.”
Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi Septemba 1996, wakati ambapo kulikuwa na ugomvi mkubwa kati yake na timu ya rapa Notorious B.I.G ikiwa chini ya lebo ya Bad Boys ya P. Diddy. Muuaji wake bado hajafahamika kufuatia upelelezi wa vyombo vya usalama. Baadaye, B.I.G pia aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika tukio ambalo linahusishwa na kisasi.
Mbali na mashabiki, rapa Jay Electrica amefunguka kupitia Twitter akimshambulia Eminem akimuunga pia na rapa 50 Cent.
“@eminem, unathubutu vipi kumtuhumu Diddy kuhusu kumuua Tupac,” ametweet Electrica na kuongeza tweets nyingine akimuonya kuwa awe mwangalifu kabla hajamharibu.
Mashabiki wametengeneza ‘meme’ nyingi zinazoonesha namna ambayo Diddy atakuwa amefanya baada ya kusikia mstari wa Eminem.
Hata hivyo, Diddy hajasema neno lolote kuhusu mstari wa wimbo huo wa Eminem.
Eminem amewashangaza mashabiki kwa ngoma hiyo aliyoiachia ghafla akijibu ile ngoma ya aliyoshambuliwa na Machine Gun Kelly kupitia wimbo wa ‘Rap Devil’.
Katika ngoma hii, Eminem amemrarua rapa huyo kinda, “Nina umri wa miaka 45 lakini nauza zaidi yako. Wimbo wangu mbovu zaidi kwako ndio wimbo wako mkali zaidi,” tafsiri ya baadhi ya mistari.
“Ni bora niwe na umri wa miaka 80 mimi kuliko kuwa wewe nikiwa na miaka 20. Haujawahi kutengeneza ngoma kali inayokaa karibu na ya Biggie, Jay, Tailor Swift au yule malay* Iggy,” maana ya mistari mingine.
Jinsi alivyolitaja jina la Iggy pia kumezua jambo na imemkasirisha rapa huyo wa kike ambaye wana ugomvi wa muda mrefu.
Isilize hapa ‘Killshot’: