Vita iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya , sasa inaanza kuonekana kumgeukia kwa kukamiwa na baadhi ya wabunge.

Baadhi ya wabunge wameonekana kuanzisha mapambano na Makonda kuhusu kutokomeza biashara ya dawa za kulevya huku wengine wakihoji uadilifu wa kiongozi huyo juu ya mali anazomiliki.

Mbunge wa Geita vijijini , Joseph Msukuma(CCM), amedai kuwa Makonda anamiliki mali nyingi zisizoendana na muda aliokaa kwenye utumishi wa umma.

”Mh. Naibu Spika, RC wa Dar es salaam mwaka 2015 alikuwa akiishi kwa Membe, lakini tangu awe RC kwa mwaka mmoja sasa anatumia Lexus yenye thamani ya milioni 400, anamiliki V8 na mwanza amejenga maghorofa ndani ya mwaka mmoja,”amesema Msukuma.

Akitoa mwongozo wake, Naibu Spika Tulia Ackson amemtaka Msukuma  kutumia kanuni nyingine ya Bunge kwakuwa kanuni ya 68(7) aliyokuwa ametumia inahusu jambo lililotokea bungeni muda mfupi na si vinginevyo.

Hata hivyo, Msukuma ametoa kauli hiyo ikiwa ni muendelezo wa kumtuhumu Makonda baada ya kufanya hivyo bungeni juzi aliposema anashangaa kuona Taifa linafanyia kazi taarifa ya Mkuu huyo wa Mkoa juu ya wauza dawa za kulevya.

 

Tulia amtaka kigwangalla kuisoma ripoti ya CAG
Video: Mbunge Lissu aligawa Bunge, Makonda akamiwa