Mamlaka ya bandari nchini Msumbiji imekanusha madai kwamba meli yake ilikuwa imebeba vifaa vilivyo sababisha mlipuko wa Beirut nchini Lebanon, kwa mujibu wa AFP.

Meli hiyo ambayo ilikuwa inatokea bandari ya Beira, nchini Msumbiji inadaiwa kuwa ilishusha mzigo Beirut na shehena ya mzigo ambao ulihifadhiwa katika ghala ya bandari.

“Mamlaka ya bandari haikuwa inajua kuwa meli ya MV Rhosus iliacha mzigo katika bandari ya Beira,” imeeleza mamlaka ya bandari ya Beira.

Inasema hakukuwa na tangazo la kuwasili kwa meli bandarini hapo ndani ya siku saba mpaka 15.

Lakini maafisa wa bandari ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wameimbia AFP kuwa ingawa meli hiyo ilikuwa imewasili katika bandari ya Beira, lakini safari yake ilikuwa haipaswi kuishia Msumbiji bali Zimbabwe au Zambia, kwa sababu ilikuwa imebeba kemikali inayotumika kutengeneza mlipuko kwa ajili ya sekta ya migodi.

Mamlaka ya bandari inayofuatilia mienendo ya Meli,imesema kuwa vyombo vya majini vinavyo pepeza bendera ya Moldoval viliwasili Beirut tangu Nov,20, 2013 na havijawahi kuondoka.

Ahukumiwa kifo baada ya kumchinja mtoto wake
Mlipuko Lebanon: Wafanyakazi 16 wakamatwa