Kwa mara ya kwanza kiungo Msuva amechezea timu ya nyumbani baada ya kusainiwa kucheza timu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ambapo katika mechi ya kirafiki aliyocheza na Botswana Msuva ameichapa mabao mawili.

Msuva alipata nafasi kuongea na vyombo vya habari amesema kuwa Samatta ni mfano mzuri wa kuigwa na wanasoka wa bongo kiwango chake na bidii yake katika mpira kimemvutia na kumfanya aongeze bidii katika soka lake.

“Samatta ametuonesha mfano fulani sisi wachezaji wa nyumbani kwa upande wangu nimefurahi Samatta kuonesha njia wengine tunafuata na tumemfuata Samatta kwa wivu wa kimaendeleo, kwa nini yeye anafanya vizuri nje lakini wakati mwingine  Samatta huwa anatuambia kila mchezaji una uwezo hiyo ilikuwa kitupatia wivu,” Msuva.

Hata hivyo amesema kuwa kupitia mchezo huo wa kirafiki, Msuva anaamini yeye kufunga katika mechi ya jana kutamuongezea nafasi nzuri ikiwepo uaminifu katika timu yake ya huko nje ya Nchi.

”Unapofunga kwenye nchi yako, timu za nje wanaongeza uaminifu kwako”. Amesema Msuva.

Msuva ameongeza kuwa, “Namshukuru Mungu kwa hatua niliyopiga na nafurahi kurudi nyumbani kulitumikia Taifa langu kwa sababu nimetoka Tanzania na nimepata timu Morocco, kiukweli nje ni nje tukiangalia mfano Samatta ametoka wakati ambao kulikuwa hakuna mchezaji anacheza nje”.

Aidha Msuva amechukua nafasi hiyo kuwatia moyo wachezaji wenzake wa hapa nyumbani na kusema kuwa kila mmoja anauwezo wa kwenda kucheza nje ya nchi hivyo wasikate tamaa na wazidi kujituma.

 

Baada ya 2Pac Chid Benz ampa shavu Jay z
Mwanahabari Muhingo Rweyemamu afariki dunia