Mkoani Kagera Wilaya ya Bukoba mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari Nyakato, Robert Masaba (21) amefariki dunia mara baada ya kujinyonga usiku wa kuamkia leo.

Mwanafunzi huyo amefariki dunia ikiwa imebaki siku moja kukaa kwenye chumba cha mtihani wa mwisho wa taifa wa kuhitimu mafunzo ya sekondari, ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani (NECTA), Charles Msonde ametangaza kuanzia kesho, Mei 7, 2018 wanafunzi wapatao 87,643 wanatarajia kuanza rasmi mitihani yao ya Taifa inayofanyika nchi nzima.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kuwa Masaba amejinyonga usiku wa kuamkia leo kwenye mwembe akiwa shule ya Sekondari Kahororo na sababu za kujinyonga mpaka kuaga dunia bado haijafahamika mara moja.

Masaba na wenzake walihamishiwa katika shule ya Kahororo baada ya shule yao ya Nyakato kuathiriwa na tetemeko la ardhi.

Aidha mkuu wa shule ya Kahororo, Omary Rugambaki amezungumzia tukio hilo akisema polisi wameshafika kwa uchunguzi zaidi.

 

Wanaume watakiwa kujitokeza kupima Ukimwi
Video: Rais Magufuli aruhusu wamachinga kufanya biashara katika kituo cha mabasi cha kisasa