Mtaji wa Taasisi ya Uwekezaji nchini – UTT AMIS, umeongezeka kwa kasi na kufikia Shilingi 1.5 trilioni katika kipindi cha miaka minne hadi kufikiwa mwaka huu wa 2023, ambayo sawa na asilimia 54.
Akizungumza katika kikao kazi baina ya Wahariri kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala amesema walianza mwaka 2009 kwa mtaji wa Shilingi 65.9 Bilioni.
Amesema, “tumekuwa na ukuaji mkubwa sana. Kila Mwaka tumekuwa tunavuka malengo yetu na faida kwa wateja wetu nayo inaongezeka kila kukicha ukilinganishwa na taasisi ilipoanza,” amesisitiza Mkurugenzi wa taasisi hiyo.
Awali, Meneja Masoko, Daudi Mbaga amesema kuwa taasisi hiyo inatoa mafao saba ambayo ni Umoja, Wekeza, Watoto, Jikimu, Liquid na Hatifungani ambapo kwasasa wastani wa faida inayopatikana katila Mifuko hiyo ni asilimia 12 kwa mwaka..
Kwa upande wake Mjumbe wa jukwaa la wahariri – TEF, Anjella Akilimali alisema mkutano na Kampuni hiyo umewafanya kuyafahamu mengi, hivyo watakuwa daraja la kuwafikishia wananchi elimu juu ya uwekezaji huo.