Mtalii Justin Kyllo (51), raia wa Canada amefariki baada ya parashuti aliyokuwa akiitumia kuruka angani kutoka katika kilele cha mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kugoma kufunguka.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amethibitisha kifo cha mtalii huyo jana, na kueleza kuwa kimetokea katika kituo cha Stella point kilichopo katika mlima huo.

Ameeleza kuwa mtalii huyo alifika Septemba 20 mwaka huu, kwaajili ya kupanda mlima, lakini jana asubuhi alitumia parashuti kwaajili ya kuruka angani ili kushuka chini ya mlima lakini iligoma kufunguka na kusababisha kifo chake.

Diamondi kutua kilele cha mlima kilimanjaro
Kipimo cha UKIMWI kwa mdomo chazinduliwa Uganda