Mtangazaji wa kituo kimoja Televisheni nchini Misri amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja mara baada ya kufanya mahojiano na mtu anayejihusisha na biashara ya ngono yaani mapenzi ya jinsia moja maarufu kama (Shoga)

Mtangazaji huyo anayejulikana kwa jina la Mohammed el-Gheiti alikumbwa na kadhia hiyo mara baada ya kipindi chake cha Augost mwaka 2018 kumhoji shoga huyo ambaye alielezea jinsi anavyofanya kazi yake.

Aidha, ushogo si kosa kisheria nchini humo lakini ni jambo ambalo halikubaliki nchini humo na kwamba huonekana ni kitendo cha ajabu kwa jamii hiyo ya waislamu wenye msimamo mkali.

Hata hivyo, ukahaba, ushoga na biashara ya ngono umekuwa ukipingwa katika nchi nyingi barani Afrika, pia ni kosa kisheria.

Video: Hawa ndiyo Marais wenye ulinzi mkubwa zaidi duniani
DC Msafiri awacharukia watumishi Njombe

Comments

comments