Mtangazaji maarufu wa televisheni nchini Zimbabwe Zororo Makamba (30)  amefariki dunia kwa ugonjwa wa Corona machi 23,2020 ambapo amekuwa mtu wa kwanza kufariki kwa ugonjwa wa Corona nchini humo ambaye ni  miongoni mwa wawili wa kwanza kubainka kuwa na virusi hivyo.

Taarifa iliyotolewa na Obadiah Moyo, Waziri wa Afya wa Zimbambwe imeeleza, Makamba alisafiri kwenda New York tarehe 29 February 2020 na kurejea Harare, Zimbabwe tarehe 9 Machi 2020 ambapo alianza kuona mabadiliko ya afya yake siku chache baada ya kurejea.

Makamba alipata virusi hivyo alipokuwa New York nchini Marekani. Baada ya kufika Zimbabwe na kufanyiwa vipimo, alitengwa na kuwekwa katika jengo pekee la Wilkins lililopo katika hospitali hiyo ya Harare, lililowekwa maalumu kwa wanaobainika kuwa na virusi hivyo.

Kwamujibu wa kituo cha habari cha CNN rafiki wa Makamba amesema, rafiki yake baada ya kurejea alikuwa akisumbuliwa na mafua makali, homa za mara kwa mara pamoja na mwili kuchoka ambapo alipelekwa katika Hospitali Kuu ya Harare, baada ya kuzidiwa na mafua huku dalili mbalimbali za ugonjwa huo zikiendelea kudhihirika.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ametangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo isipokuwa kwa raia wa nchi hiyo wanaorejea nyumbani na magari ya mizigo.

Pia amepiga marufuku mikusanyo ya watu zaidi ya 50 na kufunga baa, klabu za usiku, majumba ya mazoezi (gyms) na maeneo ya kuogelea kutokana na tishio la corona.

Fuata taratibu hizi wakati wa kunawa mikono
Video: Makonda asema mtoto wa Mbowe ana Corona

Comments

comments