Mtangazaji nguli wa mahojiano na Mfalme wa ‘Talk Shows’ wa Marekani, Larry King amefariki dunia leo, Januari 23, 2021 kwa ugonjwa wa Covid-19.

King ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 87 alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Cedars-Sinai, Los Angeles baada ya kubainika kuwa na Covid-19.

Larry King alikuwa akitangaza kupitia CNN kwa zaidi ya miongo mitatu, amefanya kazi ya media kwa miaka 63, akifanya mahojiano na zaidi ya watu 60,000, maarufu, mashuhuri, wa kati na wenye mambo mazito yaliyopaswa kuzungumziwa.

Mwaka 2010 aliachana na CNN aliyokuwa akiruka kupitia kipindi cha ‘Larry King Live’, akaingia mtandaoni na kipindi cha ‘Larry King Now’.

Aliapa kuwa hatastaafu utangazaji hasa kufanya mahojiano, hadi kifo kilipomchukua.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 24, 2021
Serikali yatoa tamako zuio la kuingia Uingereza