Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili (DW) Mohammed Dahman amefariki dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) Jijini Cologne, magharibi mwa Ujerumani.

Taarifa za kifo cha mtangazaji huyo mahiri zimetolewa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt

Mohammed Dahman alikuwa mwandishi wa habari mahiri katika nyanja zote, lakini alipendelea sana taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.

Asilimia kubwa ya wasikilizaji walizipenda sana makala zake kuhusu masuala ya haki za binadamu na sauti yake ya huruma na alikuwa makini sana katika kuhakikisha taarifa zake pamoja na makala haziegemei upande mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa DW, Andrea Schmidt imesema kuwa, Dahman alikuwa akiugua kwa kipindi cha takribani miaka miwili na muda wote huo hakuweza kufanyakazi.

”Katika wakati huu mgumu wa majaribu, fikra na dua zetu tunazielekeza kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni. Tunawapa pole na kutoa rambirambi zetu kwa majonzi makubwa, machozi yakitiririka machoni mwetu. Tunawaombea. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi.”imeeleza taarifa hiyo

 

Dkt. Bashiru awaonya viongozi wa CCM na Serikali, 'Atakayewadharau hawa huyo hatufai'
Ahukumiwa kwenda jela kwa kutoa lugha chafu dhidi Rais Museveni