Mtanzania aliyetambulika kwa jina la Msafiri Musa amekamatwa, na yupo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi Nchini Kenya (JKIA), kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya amabazo zilikuwa kwenye sehemu yake ya haja kubwa.
Taarifa zilizotolewa zimeeleza kuwa Musa na wenzake walikuwa safarini kuelekea China na India wakati walipokamatwa usiku wa kuamkia jana katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mtanznia huyo ambaye ametambuliwa na idara ya uchunguzi wa jinai nchini Kenya kama msafiri alitoa tembe 47 za dawa za kulevya kwa mara ya kwanza.
Na imelezwa kuwa baada ya kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi idara ya uchunguzi, Musa alitoa tembe nyingine 69.
Pamoja na kwamba Polisi Nchi Kenya wamemtaja Mtanznia huyo lakini hawajaweza kuwataja raia wa mataifa mengine ni wakina nani.
Aidha, idara ya uchunguzi wa jinai Kenya imesema kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’ kuwa wachunguzi wa jinai wamewasilisha maombi katika mahakama ya JKIA kumzuilia zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi wao.