Raia wa Tanzania, Basaida Zena Jaffary amehukumiwa kwenda jela miaka 5 baada ya kukamatwa akiwa na mzigo wa dawa za kulevya Kilogram 2.3, aina ya Cocaine na Heroine, zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Milioni 155
Zena Jafary ambaye ni mfanyabiashara wa chakula aliwasili nchini Ghana katika Uwanja wa Ndege wa Kotoko akitumia Ndege ya Shirika la Rwanda Air.
Aidha, maafisa wa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini humo walibaini shehena hiyo ya dawa hizo haramu zilizowekwa katika bahasha mbili.
Hata hivyo, Baada ya kuhojiwa na maafisa hao, Zena alikiri kumiliki bahasha hizo na kwamba, alipewa Mandanje Omari raia wa Tanzania na kutakiwa kuzifikisha kwa mtu mmoja anayeishi katika Jiji la Accra nchini humo.