Waziri wa Afya nchini Uganda,  Dkt. Jane Aceng amesema Aprili 17, 2020 walipima Sampuli 1,120 na moja ikagundulika kuwa na COVID 19 ambayo ni ya dereva wa gari la mizigo kutoka Dar es salaam.

Wizara imesema inafanya jitihada za kumfuatilia dereva huyo aliyeingia Uganda kupitia mpaka wa Mutukula.

”Mgonjwa mpya ni Mtanzania (34), Dereva wa Lori kutoka DSM ambaye alifika mpaka wa Mtukula April 16, 2020, tulipopima sampuli 744 za madereva mpakani yeye akakutwa na corona, tunamfuatilia ili kumrudisha Tanzania, kwahiyo idadi ya visa Uganda imebaki 55’’ amesema Waziri wa Afya Uganda

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo ya Afya ya Uagnda inaeeleza kuwa dereva huyo hakuwa na dalili zozote za ugonjwa wa COVID 19.

Aidha, hadi sasa Uganda bado inaendelea kuwa na visa 55 vya wagonjwa wa Corona kufuatia mgpnjwa mpya mmoja aliyejulikana jana kuwa si raia wa Uganga.

Makonda: Kila familia ikae kikao ijadili kuhusu Corona
Watakaokunywa pombe bar kukiona cha 'mtemakuni', DC aagiza