Binti mdogo kuliko wote Afrika kupanda Mlima Everest, ambaye pia ni Mtanzania wa kwanza Mwanamke kufikia kilele cha Mlima huo, Rawan Dakik, amesema zoezi alilofanya la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa zaidi ya mara tano limechangia kufanikiwa kwake kupanda mlima huo mrefu zaidi duniani wenye urefu wa mita 8,850 kutoka usawa wa Bahari.

Rawan ameyasema hayo leo Juni 11, 2021 mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Nepal kwenye zoezi hilo lilochukua miezi miwili, ambapo amepokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Masanja ameeleza kufurahishwa na hatua ya mafanikio ya Dakik na kuwa itakuwa njia nzuri zaidi ya kuutangaza Mlima Kilimanjaro kiutalii kama sehemu bora kwa mazoezi kwa wanaopenda kupanda milima mirefu zaidi duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amepongeza uamuzi huo wa kishujaa wa Rawan kuwa utahamasisha Watanzania wengi zaidi kupenda utalii wa kupanda milima hususan Mlima Kilimanjaro.

Dakik, alifanikiwa kufika kilele cha Mlima Everest, Mei 23, 2021 baada ya takriban miezi miwili tangu kuanza kwa safari yake hiyo aliyoianza Machi 29, mwaka huu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 12, 2021
R Kelly awafuta kazi wanasheria wake