Aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2000 na kushinda taji hilo ambaye bado anaendeleza urembo huo, Jacqueline Ntuyabaliwe kwa sasa ni mke wa tajiri mmoja hapa nchini Regnald Mengi anatajwa kuwa ni moja kati wa warembo nchini wanaomiliki mkoba wa gharama zaidi unaogharimu shilingi Milioni 60 za kitanzania.

Jackline ni moja ya wanamitindo na wapenda fashion Tanzania, mwanamke mjasiriamali na tajiri ametajwa kama moja ya wanawake wanaomiliki mkoba wenye bei kubwa Duniani ambapo kwa Tanzania inasemekana kuwa yuko peke yake.

Muonekano na muundo wa mkoba huo ni wa kawaida design yake wengi waliwahi kuwa nao , lakini hapa utofauti wa mkoba huu unakuja kuanzia nembo maarufu duniani inayotengeneza mkoba huo wenye thamani  na ubora.

Mkoba huo unaojulikana kama birkin, unaotengenezwa na kampuni ya  Hermes nchini Ufaransa na kwa mujibu wa moja ya mitandao ya kibiashara hapa Duniani wa eBay umetaja gharama ya mkoba huo unauzwa kwa Dola $26500 sawa na shilingi milion 60 za kitanzania.

Unaambiwa kwamba gharama ya pochi hiyo ni kutokana na kutengenezwa kwa kutumia ngozi ya mamba lakini pia jina kubwa la kampuni hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilianzishwa mnamo mwaka 1837 ikiwa inajihusisha na utengenezaji wa vitu vya urembo kama vile, saa, hereni, mikufu, mikoba na kadhalika Hermes ni moja ya kampuni kubwa sana hapa duniani kutokana na ubora wa bidhaa zake.

Shusha komenti yako hapo chini ukipata ngekewa ya kupewa kiasi hiko cha fedha ungetumia kufanya nini…………?

Bobi Wine aachiwa, akamatwa tena na Jeshi la Polisi
Chadema yafanya kweli Korogwe Vijijini