Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashinadano yaliyoratibiwa na programu ya kukuza ubunifu kusini mwa Afrika (Southern Africa Innovation Support Program (SAIS)) kwa kuibuka kidedea na kuwa mshindi namba moja.

Aidha Mashindano hayo yamehusisha wabunifu kutoka nchi za Afrika Kusini, Botswana, Namibia, Zambia na Tanzania, ikiwa na washiriki 11 ambapo Tanzania ilikuwa na wabunifu wawili Moses Rodgers Mbagaambaye amebuni mfumo wa si,u na tovuti ujulikanao kama Exam Net, na Godfrey Gervas ambaye ni mshindi mwazilishi mwenza na kiongozi wa kampuni inayotokana na ubunifu iitwayo Fundi App inayomwezesha mwenye mahitaji ya ufundi kupata huduma ya upatikanaji wa mafundi kupitia mfumo wa simu za kiganjani.

Akizungumza na wandishi wa habari Mkurugenzi wa COSTECH Dkt Amos Nungu amesema kuwa kupitia ushindi huo umeiweka Tanzania katika nafasi ya kufahamika zaidi kimataifa.

Kwa upande wake mshindi Godfrey amesema kuwa kupitia mashindano hayo wamejifunza mengi lakini pia fursa nyingi zimejitokeza ambapo mpaka sasa wamepata kampuni tatu zilizotaka kufanya nao kazi, katika upande wa zawadi amepata zawadi yenye thamani ya kiasi cha shilingi miloni 8

JoeBoy awalilia waandaji wa tamasha la Afro Jam 'Kenya
Maofisa 747 wa Polisi wahitimu mafunzo