Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara inaelekea ukingoni. Ligi hiyo itakayotoa washindani watatu wapya katika ligi kuu msimu wa 2016/17, imegawanywa katika makundi matatu na kila mshindi wa kundi atapanda moja kwa moja VPL msimu ujao.

KUNDI C:

Dar es Salaam wanaweza kupata timu nyingine katika ligi kuu msimu ujao. Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’, African Lyon, timu ya Manispaa ya Kinondoni, KCMC, Friends Rangers zote zina nafasi ya kupanda.

lakini zikiwa zimesalia mechi tatu kwakila timu, Ashanti wanakamata kilele cha kundi wakiwa na alama 22, Lyon inafuatia kwa karibu sana ikiwa na pointi 20, KCMC na Rangers zinafuatia zikiwa na alama 17 kila timu katika nafasi za tatu na nne.

Kiluvya United ya Pwani inashikilia nafasi ya 5 ikiwa na pointi 16 (
ki-hesabu inaweza kupanda pia) Polisi Dar FC iliyo nafasi ya 6 inapaswa kupambana sambamba na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma ili kutoshuka daraja.

Polisi Dodoma FC ambayo imehamishwa kutoka Dodoma hadi Mpwapwa ni kama tayari imeteremka daraja kwani imefanikiwa kukusanya alama 3 tu hadi hivi sasa

Kama Itakua Hivi, Suleimani Matola Atakua Na Bahati Ya Kipekee
Diamond afichua kuwa ana mtoto mwingine tofauti na 'Tiffah'