Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa agizo la kusitishwa kuchezwa kwa video ya wimbo wa msanii Diamond Platnumz aliomshirikisha Zuchu ‘Mtasubiri Sana’ kufuatia kuwepo kwa sehemu ya video hiyo kumuonyesha Zuchu akiwa Kanisani anaimba kwaya na baadae kuacha na kukimbilia mapenzi.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na TCRA kuelekea kwa vyombo mbali mbali vya utangazaji imefafanua kuwa tatizo kubwa lilisababisha kusitishwa kwa video hiyo ni sehemu inayomuonyesha Zuchu akiwa kanisani kama mmoja wa waimbaji wa kwaya ambaye alionekana na baadae video ikaendelea kwingine.

” Katika video hiyo kuna kipande kimeonyesha wahusika wapo kanisani wanaimba kwaya lakini baadae wakaacha na kuelekea kwingine, kipande hicho cha video kimeleta ukakasi miongoni mwa Waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kwamba ni dharau juu ya dini/madhehebu fulani.

Hivyo kwa barua hii TCRA inaagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii hapa nchini kutorusha video ya wimbo uitwao ‘Mtasubiri sana’ ulioimbwa na msanii Nasib Abdul (Diamond Platnumz) kwa kushirikiana na Zuhura Othman Soud (Zuchu), hadi hapo atakaporekebisha sehemu hiyo ya video.”

TEITI yawapiga msasa viongozi kwenye uziduaji
Waziri atoa onyo kupandisha bei kiholela 'ni kosa la jinai'