Mtawa mmoja nchini Marekani amefungwa jela mwaka mmoja baada ya kukiri kuiba pesa zaidi ya milioni 90 ya kitazania kutoka shule ya California ambako alihudumu ili kufadhili michezo yake ya kamari.

Mary Margaret Kreuper, mtawa mstaafu, mwenye umri wa miaka 80, atatumikia kifungo cha mwaka mmoja na siku moja kwa ulaghai wa kuiba pesa kupitia njia ya elektroniki na utakatishaji fedha.

Imeripotiwa kuwa Kreuper aliiba pesa hizo kutoka kwenye masomo na michango iliyotolewa kwa Shule ya Kikatoliki ya St James ambapo alikuwa mkuu kisha aliwaagiza wafanyakazi wengine wa shule hiyo kubadilisha na kuharibu rekodi za kifedha ili kuficha uhalifu wake.

Kulingana na waendeshaji mashtaka, pesa hizo ambazo zingeweza kulipa karo ya zaidi ya wanafunzi 12, zilitumika kwenda kasino na likizo kwa Kreuper na marafiki zake.

Akikiri makosa yake, Kreuper alisema, “Nimetenda dhambi, nimevunja sheria na sina visingizio. Nimesikitika sana na ningetumia maisha yangu yote kujaribu kufuata kwa ukaribu zaidi katika nyayo za Kristo.”

Mpango huo ulifichuliwa wakati wa ukaguzi baada ya Kreuper kustaafu mwaka 2018. Akitoka hukumu yake, Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani, Otis D Wright II, alimfunga jela Kreuper mwaka mmoja na siku moja na pia kumuamuru alipe shule hiyo KSh 94,881,050.

Dkt.Mabula aapishwa rasmi kuwa Waziri wa Ardhi
Nelly aomba radhi kwa video chafu