Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Simba, Mtemi Ramadhani ameamua kujiondoka katika kinyang’anyiro hicho.

Amesema kuwa sababu zilizomfanya aondoe jina lake kugombea uenyekiti wa klabu ya Simba huku uchaguzi ukiwa umepangwa kufanyika mwezi ujao amesema kuwa anaweza kuhamia Dodoma, hivyo hataweza kuitumikia nafasi yake vizuri.

Amekiri kuwa ni kweli ameandika barua kwenda kwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba, kwamba anaomba jina lake liondolewe kwenye kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba.

“Sababu kubwa sasa hivi nina majukumu mengi, ninaweza kuhamia Dodoma kwa hiyo nadhani sitaweza kuitumikia vyema klabu yangu ya Simba, lakini pia ningependa kuona klabu ina umoja katika kipindi hiki ambacho tunatarajia kutetea ubingwa wetu ambao tuliupata msimu uliopita.”amesema Mtemi Ramadhan

Aidha, amesema kuwa mara nyingi chaguzi hizo zimekuwa zikiwagawa wanachama, hivyo amesisitiza kuwa kipindi hiki wanahitaji umoja.

Kujiondoa kwa Mtemi Ramadhani inamaanisha kuwa, Sued Nkwabi anabaki peke yake kugombea nafasi ya uenyekiti wa Simba kwa sababu kwa muda uliosalia hauruhusu mtu mwingine kuingia kugombea.

 

FA wamuongezea muda Jose Mourinho
Video: Mke amsaliti mumewe, wafanya utekaji kwa miaka 7