Taarifa kutoka Maungu Turiani mkoani Morogoro zinaeleza kuwa Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar ukavunja mkataba na Kocha Mkuu Salum Mayanga kutokana na kuwa katika mazingira magumu wa ya kupata matokeo yasiyoridhisha.

Mayanga alijiunga na timu hiyo katikati ya msimu uliopita akitokea Tanzania Prisons ambayo haikuwa na matokeo mazuri.

Hata hivyo Mtibwa Sugar ilikuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi Kuu msimu huu 2022/23 lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kutokana na kupoteza mechi mfululizo na kuiweka nafasi ya 11 ikiwa na alama 29 kati ya timu 16.

Katika mechi sita za mwisho imeshinda mchezo mmoja dhidi ya KMC bao 1-0 kisha kupoteza mitano dhidi ya Singida BS, 2-0, Simba 3-0, Azam iliyoshinda 2-0 (Kombe la FA).

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Swabri Aboubakari amesema bado hawajaachana na kocha huyo isipokuwa wanaendelea na mazungumzo naye ya mwisho kujua sababu za kutokuwa na matokeo mazuri.

Amesema watakapokamilisha majadiliano na kubaini tatizo watatoa taarifa rasmi kama wameachana naye au kuendelea kuiongoza Mtibwa Sugar na kusisitiza bado wanamtambua kama kocha wao.

“Siwezi kusema tumemalizana naye kwa sasa ila tuko katika majadiliano ikifikia mwisho tutaweka wazi, ila ieleweke hadi sasa bado ana mkataba na Mtibwa Sugar,” alisema Aboubakari.

Kigogo huyo aliongeza, sababu kubwa ya kufikia hatua hiyo ya kumweka kwenye vikao nyota huyo wa zamani wa timu hiyo ni kutokana na mwenendo wa matokeo yasiyoridhisha.

Miundombinu huduma za Elimu, Afya kwa jamii yaimarishwa
Jafo azindua miradi Mvomero, ataka Wananchi waitunze