Mabingwa wa Soka Tanzania bara msimu wa 1998/99 na 1999/2000 Mtibwa Sugar wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumpata Mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Seif Karihe ili akaitumikie msimu ujao huku ikielezwa ni pendekezo la kocha mkuu wa timu hiyo, Habib Kondo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Swabri Aboubakar amesema wachezaji wote waliopendekezwa na benchi la ufundi wameanza nao mazungumzo ya kuwaongeza kikosini mwao.

“Tumeondokewa na wachezaji wengi ila sio sababu ya sisi pia kushindwa kusajili wachezaji wengine nchini, tunaamini usajili wetu wote utakapokamilisha basi mashabiki wetu watafurahi,” amesema

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson akizungumzia kama wameachana na nyota huyo amesema: “Kwa sasa tunaangalia jinsi ya kuboresha kikosi chetu hivyo kwa wachezaji wote ambao tutawaacha basi tutawatangaza kwenye vyanzo vyetu, tuvumiliane tu kwa sababu bado muda ni mrefu.”

Endapo dili hilo litakamilika basi Karihe ataenda kuungana na mastaa wengine wakiwemo, Kelvin Nashon na Yassin Mustapha waliotokea Singida Fountain Gate na Matheo Anthony aliyeachana na KMC.

Romelu Lukaku achoshwa na kelele za usajili
Bernardo Silva abembelezwa Man City