Idara ya Habari na Mawasilino ya Mtibwa Sugar imewatoa hofu Mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguuko wa 23, dhidi ya Singida Big Stars.

Mtibwa Sugar itacheza ugenini Uwanja wa Liti mkoani Singida keshokutwa Jumatatu (Februari 27), dhidi ya Singida Big Stars ambayo imedhamiria kumaliza nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Mkuu wa Idara ya Habari Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kikosi chao kinaelekea mkoani Singida, kikiwa na matarajio makubwa na kuvuna alama tatu muhimu, hivyo mashabiki wanapaswa kuwa na imani na wachezaji wao.

Kifaru amesema katika mchezo huo Benchi la Ufundi na Wachezaji kwa ujumla wamekubaliana kupambana kikamilifu ili kuendeleza moto wa ushindi, kama walivyofanya dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao walikubali kufungwa 1-0, Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro juma lililopita.

“Tuna imani mchezo huu tutashinda japo tunajuwa utakuwa mgumu kwa kiasi chake, tuna matumaini makubwa kutokana na matokeo ya mchezo wetu uliopita dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao ulimalizika kwa ushindi wa 1-0.”

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Singida Big Stars, tunawaheshimu kwa sababu wanacheza Ligi Kuu kama sisi, lakini niwahakikishiea Mashabiki wa Mtibwa Sugar timu yao ipo vizuri na tayari kwa kuziwania alama tatu katika Uwanja wa ugenini.” amesema Thobias Kifaru

Mtibwa Sugar inakwenda kupambana mkoani Singida ikiwa nafasi ya tisa kwa kumiliki alama 29 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku wenyeji wao SIngida Big Stars wakiwa nafati ya nne kwa kufikisha alama 44 sawa na Azma FC.

Simba SC yashikili ajira ya Kocha Vipers SC
Singida Big Stars yaitambia Mtibwa Sugar