Wakata Miwa kutoka Manungu Turiani mkoani Morogoro ‘Mtibwa Sugar’ wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2021-21, kwa kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano (Play Off) dhidi Transit Camp FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 4-1, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, huku Mshambuliaji mzawa kutoka visiwani Zanzibar Ibrahim Hilika akifunga mabao matatu pekee yake.

Bao lingine la Mtibwa Sugar katika mchezo huo limefungwa na Kelvin Kongwe Sabato huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Karegea Waranga.

Mchezo wa mkondo wa pili kwa timu hizo utapigwa Julai 24 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na matokeo ya jumla yataamua ima Mtibwa Sugar ibaki Ligi Kuu ama kushuka hadi Daraja la Kwanza, au Transit Camp FC ibaki Ligi Daraja la Kwanza au ipande Ligi Kuu msimu ujao 2021-22.

Al Ahly yamuwinda Luis Miquissone
Coastal Union bado inaitaka Ligi Kuu