Jeshi la polisi Kisumu, nchini Kenya, limewatia mbaroni wazazi wa mtoto wa  kiume wa miaka 14, kwa kumchoma moto viganja vya mikono yake kwa tuhuma za kupoteza simu ya mkononi.

Mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la 8 ambao wanatarajiwa kufanya mitihani ya taifa ya kumaliza shule ya msingi inayoanza jumanne wiki ijayo.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi, Leonard Matete wazazi wote wawili wamehojiwa ili kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo.

Mtoto huyo ambaye mama yake alifariki akiwa na umri wa mwaka mmoja, amekuwa akiishi na baba yake na mamayake wa kambo, Rose Akoth.

Imeelezwa kuwa, mama huyo alimzungushia magazeti kwenye viganja vya mikono na kumfunga na kamba kisha kumwagia mafuta ya taa na kumchoma.

Mumewake Onjoro Omuya, alijaribu kufanya kila njia ili kuficha tukio hilo lisijulikane na taarifa za upelelezi zinaeleza kuwa walimkataza mtoto huyo asimwambie mtu kilicho tokea.

Afisa wa polisi wamempeleka mtoto huyo hospitali kwa matibabu zaidi na baada ya hapo watampeleka kituo cha kulea watoto ili ajiandae na mitihani ya taifa wiki ijayo.

 

 

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 25, 2019
Harmonize asimulia alivyopokea simu ya Rais Magufuli usiku, aahidi kuwa mbunge