Mtoto mwenye umri wa miaka 5 aliyenasa kwenye kisima nchini Morocco kwa siku nne amekutwa amefariki dunia, hata baada ya jitihada kubwa na ya hatari iliyofanywa na nchi hiyo kumwokoa.
Tamko lililotolewa na Utawala wa Kifalme nchini humo, limesema kifo chake kimetokea mda mchache mara tu alipookolewa kutoka kwenye kisima hicho.
Jitihada za kuokolewa kwa mtoto huyo aitwaye Rayan kulisikitisha taifa hilo huku mamia wakifuatilia uokoaji huo eneo hilo na wengine kwa vyombo vya habari na mtandaoni.
Mtoto huyo alinasa kwenye kwenye kisima kwenye mpenyo mwembamba wa urefu wa mita 32.Kazi hiyo ya uokoaji ilifanywa Kuwa ngumu zaidi kutokana na wasiwasi wa kuporomoka kwa udongo Katika eneo hilo