Mwili wa mtoto wa miaka 6 anayefahamika kwa jina la Godluck Mfugale aliyepotea wiki mbili zilizopita mkoani Njombe, umekutwa katika poli lililopo karibu na shule ya Sekondari Njombe (NJOSS) ukiwa umeharibika.
Akizungumza wakati wa Ibada ya kuuaga mwili huo iliyofanyika katika kanisa la KKKT mjini Njombe, mchungaji wa jimbo la Njombe, Bernad Sagaya amesema kuwa mwili wa mtoto huyo ulipatikana ukiwa umeharibika hali ambayo imewashtua wakazi wa mji wa Njombe kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya mauaji ya watoto.
Aidha, kiongozi huyo wa kanisa amewaomba waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi kushirikiana na kuunga mkono jitihada ambazo zinaendelea kufanywa na viongozi wa serikali katika kukabiliana na wanaohusika na vitendo hivyo.
“Niombe tusaidiane kuweka ulinzi wa kutosha maana wanaofanya matukio haya ni vijana wetu na mimi sielewi kama watakuwa ni wazee kama mimi, yaani hawa watakuwa ni vijana wadogo wanaotafuta maisha kwa hiyo wanajaribu kila eneo kama wanaweza kufanikiwa,”amesema Mchungaji Sagaya
Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwemo Erasto mpete waliohudhulia katika mazishi ya mtoto huyo wameonyesha kusikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa mtoto huyo kwani imekuwa ni tofauti na desturi za wananchi wa mkoa wa Njombe.
-
Video: JPM awajaza noti wastaafu, Makonda aibua dude Dar
-
LIVE: Rais Magufuli akipokea ndege nyingine ya Tanzania
-
‘Kwanini tumsifie JPM wakati hizi ni kodi zetu?’, Kakobe afunguka
Hata hivyo, mpaka sasa zaidi ya watoto wanne mkoani Njombe wamepoteza maisha kwa kuuawa kikatili ndani ya miezi miwili huku matukio hayo yakiendelea kuongezeka hali inayofanya kuhusishwa na vitendo vya ushirikina