Mtoto mmoja nchini Ureno amezaliwa kutoka kwa mama aliyekufa ubongo miezi mitatu iliyopita, baada ya kufanyiwa oporesheni na madaktari katika hospitali ya Neonational iliyopo nchini humo.
Mtoto Salvador amezaliwa baada ya kukaa tumboni kwa mama yake miezi nane (wiki 32), licha ya kuwa alikuwa amekufa ubongo tokea mwezi wa Novemba akiwa na kilogram 1.7.
Maerhemu Catarina Sequeria (26), mama mzazi wa mtoto Salvador, alikuwa mwanamichezo wa kimataifa anayewakilisha taifa lake katika michezo ya mbio za boti.
kifo cha Catarina kilithibitishwa na Madaktari baada ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu akiwa nyumbani kwake mwaka jana.
Hii ni mara ya pili kwa mtoto kuzaliwa na mwanamke aliyekufa ubongo nchini Ureno, ambapo kwa mwanamichezo huyo aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa pumu tokea alipokuwa mdogo alipata shambulio alipokuwa na mimba ya miezi minne na nusu na kuwekwa chumba cha watu mahututi (ICU).
Hataa hivyo haliyake iliendelea kuwa mbaya, akathibitishwa kufariki Disemba 26, 2018, na kwa siku zilizobakia 56 aliwekewa kifaa maalumu ( Ventilator) kwaajili ya kusaidia mtoto aendelee kuishi kwenye tumbo lake hadi alipotolewa jana akiwa salama.
Kwamujibu wa mkuu wa maadili wa hospitali hiyo, Filipe Almeida, amesema kuwa uamuzi wa kumuacha mtoto ndani ya marehemu ulikubaliwa na familiya yake pamoja na mumewake ambaye alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kupata mtoto.
Mama wa marehemu Catarina, Maria de F’atima, ameviembia vyombo vya habari kuwa alimuaga marehemu tokea mwezi Disemba na mjukuu wake aliyezaliwa amekuwa faraja kwao na wanatarajia ataruhusiwa baada ya wiki tatu.