Baada ya kujizolea umaarufu mitandaoni kwa uwezo wake mkubwa hesabu, mtoto Charles Mathias aliyepata ufadhili wa kusomeshwa katika shule binafsi ya Fountain Gate Academy iliyopo jijini Dodoma ameanza rasmi masomo yake.

Charles, mwenye umri wa miaka sita ni mzaliwa katika Kijiji cha Nyigwa mkoani Morogoro, akiwa mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto watano.

Mapema mwaka huu Charlles alipata umaarufu mitandaoni baada ya kusambaa kwa video inayoonesha uwezo wake wa kuchanganua hesabu mithili ya kikokotozi, uwezo ambao uliwastaajabisha wengi kiasi cha kuzua mijadala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Charles ameanza rasmi masomo jana Aprili 12, 2021 ikiwa ni siku yake ya kwanza kuwa darasani katika shule yake mpya akianzia darasa la kwanza.

Mathias anaungana na watoto wengine 30 wenye vipaji mbalimbali ambao wanafadhiliwa na shule hiyo.

Rais Mwinyi atumbua vigogo idara maalum
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 13, 2021