Jeshi la Polisi Mkoani Njombe, linamshikilia Grace Kiumbu (30), ambaye anadaiwa kuwa mgonjwa wa afya ya akili kwa tuhuma za kumjeruhi Baba yake mdogo, Tiles Kiumbu (60), kwa kuzikata sehemu zake za siri.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe, Hamisi Issah amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Kijiji cha Idindilimunyo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe na alimkata sehemu hizo za siri wakati baba yake huyo mdogo akiwa amelala.
Amesema, “Wanasema huyu Grace ana tatizo la ugonjwa wa akili lakini yeye anajieleza anasema anatibiwa muda wote hapa kwa Baba yake anayedaiwa kuwa ni Mganga wa kienyeji, lakini safari hii alitoa Shilingi laki moja ya tiba bila mafanikio,
Mtuhumumiwa huyo pia anadaiwa kushangaa kuona watu wanaserebuka na kulewa pombe huku afya yake ikizorota hivyo Baba yake alipolala katika mkeka ilikuwa rahisi kwake kufanya tukio hilo.