Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imempokea na kuanza kumfanyia uchunguzi mtoto mwenye tatizo la utata wa jinsia na pia tundu kwenye kitovu.
Kwa mujibu wa Ofisa habari wa hospitali ya Muhimbili, Neema Mwangomo amethibitisha kupokelewa kwa mtoto huyo kutoka wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo kwasasa yupo wodini anaendelea kufanyiwa vipimo mbalimbali kubaini matatizo yake na namna ya kumsaidia.
Aidha, Mama wa mtoto huyo aliomba msaada katika vyombo vya habari ili asaidiwe kupata matibabu ya mtoto wake.
Hata hivyo, mtoto huyo mwenye umri wa miezi 18 alikuwa analia sana kwasababu korodani zake zilikuwa zikivimba na kumsababishia maumivu makali, pia ana tundu kwenye kitovu ambalo akinywa maji yanatoka,
Wazazi wake waligundua matatizo ya mototo wao mwaka jana lakini wamechelewa kumpeleka hospitali kwa kukosa fedha, ambazo kwasasa wamechangiwa na wasamalia wema na matumaini ya kupona kwa mtoto wao yamerejea.