Mwanafunzi wa Darasa la Tatu, Shule ya Msingi Ikelu iliyopo Makambako, Claud Florence (9) amefariki Dunia baada ya kujinyonga akiwa anacheza na wenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amesema Claud alikwenda shambani na Wazazi wake na wadogo zake watatu na akiwa huko alianza kucheza na wadogo zake kwa kutumia kikoi na kuanza kujaribisha namna mtu anavyojinyonga.

Kamanda Issah amesema Claud alifanya kitendo hicho katika mti pori uliopo shambani na matokeo yake alining’inia kwenye mti huku Wazazi wakiwa hawana taarifa yoyote.

Kwa mujibu wa Kamanda Issa wazazi hao walipofika walifungua hicho kikoi na kumkuta mtoto wao akiwa taabani na kumpeleka hospitali ambapo baadaye alifariki dunia.

Kamanda Issa amewataka Wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao kwani malezi ya watoto ni pamoja na kuangalia aina ya michezo wanayocheza katika mazingira yanayofaa.

“Watoto hawa wamecheza michezo ya kupitiliza mpaka wamejaribisha kujinyonga na mwenzao mmoja kujiua kabisa,” amesema Kamanda Issah.

Rais Samia atuma ujumbe wa Ramadhani
Waziri Bashungwa awatuliza Wanahabari