Mtoto wa Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi cha England ‘The Three Lions’ Harry Kane huenda akaitumikia Timu ya Taifa ya Ujerumani endapo atabarikiwa kipaji cha kusakata kabumbu.

Mpango huo umefahamika baada ya Mshambuliaji huyo kuhamia FC Bayern Munich mwishoni mwa juma lililopita akitokea Tottenham Hotspurs, huku mkewe akiwa Mjamzito, na kuna uwezekano akajifungua akiwa mjini Munich.

Mshambuliaji huyo amefichua siri kuwa, mkewe anatarajia kujifungua majuma machache yajayo, lakini aligoma kusema hospitali ambayo atajifungulia.

Pia Harry Kane amekiri mengi yalizungumzwa kutokana na uhamisho wake kwenda Bayern uliogharimu Pauni 104 Milioni.

Chanzo cha habari kimeripoti kuwa mke wa Mshambuliaji huyo anayefahamika kwa jina la Kate alisaka nyumba ya kuishi na hospitali atayokwenda kujifungua tangu mwezi Julai, mwaka huu na moto wake anaweza kuzaliwa katika jiji la Munich.

Sasa baada ya mtoto huyo kuzaliwa atakuwa na haki ya kumiliki uraia wa nchi mbili na akiwa mchezaji anaweza kuchagua timu ya taifa atakayopenda kuichezea kati ya England au Ujerumani.

Elimu: Serikali yawaita wadau wa maendeleo
Yafahamu maeneo matano ya kuogofya zaidi Duniani