Mtoto mwenye umri wa miaka mitano Jude Foley amenusurika kifo baada ya kumeza vyuma 52 kutoka kwenye kifaa cha kuchezea.

Madaktari walilazimika kumfanyia upasuaji wa tumbo katika sehemu tano ili kuondoa vyuma vilivyokuwa vimekwama tumboni mwake.

Lyndsey Foley mama wa mtoto huyo amesema alihofia kuwa mtoto wake angefariki na kutoa rai kwa wazazi wenzake kuwa makini wanapowanunulia watoto vifaa vya kuchezea.

Foley, mwenye umri wa (34), alisema alianza kuwa na wasiwasi baada ya mtoto wake kushindwa kupona baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.


Mvulana huyo alilazimika kupasuliwa tumbo sehemu tano ili kuondoa vyuma 52 vilivyokua vimekwama tumboni mwake. Picha: BBC. Chanzo: UGC

Hata hivyo wakati hali ya mwanawe ikiendelea kuzorota, alimpeleka mwanawe Jude katika hospitali ya Prince Charles mnamo Agosti 2022, akiwa na maumivu makali.

Alipomfikisha katika hospitali hiyo, uchunguzi na kipimo cha X-ray kilibaini kuwa alikuwa na vyuma tumboni.

Wizara ya afya ya Wales (PHW) imewatoa wito kwa watu kuwa makini na kufikiria kabla ya kununua bidhaa kwa ajili ya watoto wao zenye vyuma vidogo na betri na vifungo.

Lionel Messi kuongeza mmoja Paris Saint-Germain
Kocha Mgunda aukubali mziki wa Kagera Sugar