Mtoto wa muigizaji wa Fast and Furious, Paul Waker anayefahamika kwa jina la Meadow Rain Walker anashitaki kampuni ya magari iliyounda gari aina ya Porsche Carrera GT aliyopata nayo ajali baba yake na kupelekea kifo chake kwa madai kuwa ilibainika kuwa na kasoro.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 16, ameeleza katika shitaka hilo kuwa kasoro zilizobainika kwenye gari hilo ni pamoja na kuonesha kuwa ilionesha kuwa Paul Walker alinaswa ndani ya gari baada ya kupata ajali na kwamba gari hilo lilikosa mfumo madhubuti wa kuzuia moto baada ya kupata ajali.

Kwa mujibu wa TMZ, mtandao huo umeona nyaraka za kesi hiyo na kwamba zimeonesha ushahidi wa kasoro zilizobainika.

Muigizaji huyo wa Fast and Furious, Paul Walker alifariki baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Santa Clarita, Calfornia, November 2013 akiwa na rafiki yake.

Mourinho Aelekeza Vijembe FA
Jack Grealish Aitosa Ireland Ya Kaskazini