Kufuatana na mlolongo wa kesi zinazomkabili msanii wa muziki Marekani R.kelly na kudaiwa kufilisika mtoto wake Joan Lee amefukuzwa chuoni anakosoma kutokana na kutomaliziwa kulipiwa ada ya chuo.

Imeelezwa kuwa juzi Joan alifika shule na kuzuiliwa kuingia darasani kutokana na madai hayo ambapo meneja wa R.kely, Darell Johnson ametoa taarifa kuwa si kwamba R Kelly ameshindwa kulipia ada hiyo bali mwanae Joan aliamua kuacha chuo tangu mwaka 2018.

Kwa mujibu wa meneja huyo amesema kuwa R. kely yupo tayari kulipia ada ya shule lakini mpaka atakapoona mtiririko wa malipo ya fedha na kuona kama kweli fedha hizo zinafika shuleni hapo.

Inaripotiwa kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya R. Kelly na binti yake huyo toka kuachiwa kwa makala ya “Surviving R.Kelly na kudaiwa kuwaR.Kelly amekuwa akimtupia lawama mama wa mtoto huyo na kudai kuwa anampandikiza chuki binti yake.

Aidha, R Kelly ni moja ya wasanii waliopitia misukosuko mikubwa kutokana na kesi ambazo zimekuwa zikimkabili za kudhalilisha wanawake kingono, hali ambayo imefanya kupoteza mashabiki wake wengi ambao wameshindwa kuhudhuria shoo zake ambazo amekuwa akiziandaa mara baada ya kuachiliwa huru kwa dhamana kufuatia kesi hizo.

 

Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako
Video: HATARI HII…! Shuhudia MAZISHI YA AJABU ZAIDI Duniani

Comments

comments